Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa. Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.
Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi.
Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.
Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 3o tu. Hii si haba,kuna ukweli basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa.
[Soma pia: Madhara ya Mwezi Katika Hisia na Tabia za Binadamu:Kuna Ukweli? , Nyota na Kazi Zenye Mafanikio ]
Tabia Za Watu Na Alama Za Nyota
Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.
Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.
Alama hizi ni kama ifuatavyo:
1. Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20
2. Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19
3. Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21
4. Mapacha :(Gemini ): Mei 22 – Juni 20
5. Kaa(Cancer): Juni 21 – Julai 22
6. Simba (Leo): Julai 23 – Agosti 22
7. Mashuke (Virgo):Agosti 23 – Sept 22
8. Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22
9. Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21
10. Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21
11. Mbuzi (Capricorn):Des 22 – Jan 19
12. Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18
Makundi Ya Alama Za Nyota:
Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika elementi 4 zijulikanazo kama:
Moto: Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
Maji: Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
Hewa: Imara na yenye kukuza au kuendeleza
Udongo: Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha
Hizi ni elementi nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.
Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:
Moto : Kondoo, Simba,Mshale
Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
Hewa: Mapacha, Mizani, Ndoo
Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi
IJUE NYOTAYAKO
NYOTA
JINSI YA KUFAHAMU NYOTA YAKO CHUKUA JINA LA BABA YAKO CHUKUA JINA LAKO NA LA MAMA GAWANYA
KWA KUMI NA MBILI.
1. IKIBAKI MOJA NI PUNDA.
2. IKIBAKI MBILI NI NG,OMBE.
3. IKIBAKI TATU NI MAPACHA.
4. IKIBAKI NNE NI KAA.
5. IKIBAKI TANO NI SIMBA.
6. IKIBAKI SITA NI MASHUKE .
7. IKIBAKI SABA NI MIZANI .
8. IKIBAKI NANE NI NGE.
9. IKIBAKI TISA NI MSHALE.
10. IKIBAKI KUMI NI MBUZI.
11. IKIBAKI KUMI NA MOJA NI NDOO.
12. IKIBAKI KUMI NA MBILI NI SAMAKI.
NA PIA KUNA NYOTA ZA AINA NNE AMBAZO NDIZO NYOTA ZA ASILI NA UKITAKA KUZIJUA NYOTA HIZO UNACHUKUA JINA LAKO LA BABA NA LA MAMA UNAGAWANYA KWA NNE
1. IKIBAKI MOJA NI MOTO .
2. IKIBAKI MBILI NI UDONGO.
3. IKIBAKI TATU NI UPEPO.
4. IKIBAKI NNE NI MAJI.
NYOTA HIZI NDIZONYOTA ZA ASILI AMBAZO INATAKIWA TUZIFAHAMU MFANO MTU MWENYE NYOTA YA MOTO HATAKIWI KUFANYA KAZI ZA MTU MWENYE NYOTA YA MAJI
MAANA NYOTA YAKE ITAZIMIKA.
MWENYE NYOTA YA MOTO KAZI ZAKE NI UDREVA,UASKARI,UMACHINGA,HOTELI,, BIASHARA, ZINAZOHUSIKANA NA KUSAFIRI SAFIRI AU SALUNI MAANA SALUNI MOTO UNATUMIA UMEME ,FUNDI WELDING,NA KAZI ZINAZOHUSU UPEPO MAANA MOTO NA UPEPO ZIKO PAMOJA.
NA PIA NYOTA YA MAJI NA UDONGO ZINAFANYA KAZI MOJA.KAZI ZAO NI UVUVI,KULIMA ,UFUGAJI,KUCHIMBA MADINI, FUNDI WASH,FUNDI UJENZI.N.K.
MTU MWENYE NYOTA YA MOTO INATAKIWA AOLEWE NA MTU MWENYE NYOTA YA UPEPO.
NA MTU MWENYE NYOTA YA MAJI INATAKIWA AOANE NA NA MTU MWENYE NYOTA YA UDONGO.
WATU WENGI NDOA ZAO HUHARIBIKA MAANA HAWAFATI MAMBO HAYA .KUJUA NYOTA NI MUHIMU SANA NA HATA KIBIASHARA INATAKIWA TUJUE NI HERUFI GANI ZA KUANDIKA KATIKA BIASHARA AU KATIKA MADUKA YETU.
`
PIA KUNA KUZIJUA NYOTA KWA KUTUMIA HERUFI MFANO MWENYE HERUFI INAYOANZA NA A,=PUNDA.
B=NG,OMBE. C=MAPACHA. D= KAA. E= SIMBA. F=MASHUKE.
G=MIZANI . H=NGE. I=MSHALE.
J==MBUZI. K= NDOO. L=SAMAKI.
M=PUNDA. N=NG,OMBE.
O=MAPACHA. P=KAA. Q=SIMBA.
R=MASHUKE. S=MIZANI. T=NGE.
U=SAMAKI. V=MBUZI. W=NDOO.
X=SAMAKI. Y=PUNDA.
Z=NG,OMBE..NA HIZO NI KUZIJUA NYOTA KWA KUTUMIA HERUFI YA MWANZO WA JINA LAKO.
PIA KUNA KUZIJUA NYOTA KWA KUZALIWA KUTOKANA NA MWEZI ULIOZALIWA MFANO.
TAREHE 19 MWEZI WA 1 HADI
TAREHE 20 MWEZI WA 2 NI
NDOO.
TAREHE 21 MWEZI WA 2 HADI
TAREHE 20 MWEZI WA 3 N I
SAMAKI.
TAREHE 21 MWEZI WA 3 HADI
TAREHE 20 MWEZI WA 4 NI
PUNDA.
TAREHE 21 MWEZI WA 4 HADI
TAREHE 20 MWEZI WA 5 NI
NG,OMBE.
TAREHE 21 MWEZI WA 5 HADI
TAREHE 20 MWEZ I WA 6 NI
MAPACHA.
TAREHE 21 MWEZI WA 6 HADI
TAREHE 20 MWEZI WA 7 NI KAA.
TAREHE 21 MWEZI WA 7 HADI
TAREHE 21 MWEZI WA 8 NI
SIMBA.
TAREHE 22 MWEZI WA 8 HADI
TAREHE 22 MWEZI WA 9
NI MASHUKE.
TAREHE 23 MWEZI WA 9 HADI
TAREHE 22 MWEZI WA 10
NI MIZANI.
TAREHE 23 MWEZI WA 10 HADI
TAREHE 21 MWEZI WA 11
NI NGE.
TAREHE 22 MWEZI WA 11 HADI TAREHE 21 MWEZI WA 12 NI
MSHALE.
TAREHE 21 MWEZI WA 12 HADI TAREHE 18 MWEZI WA KWANZA NI
MBUZI.
HIZO NDIZO NYOTA KWA NJIA YA TAREHE .
PIA NYOTA HIZI ZIKO KATIKA MAGURUDUMU KAMA NILIYOYATAJA HAPO NYUMA MFANO.
1. NDOO= MOTO
2. PUNDA = MOTO.
3. NG,OMBE =UDONGO
4. MAPACHA = UPEPO.
5. KAA=MAJI.
6. SIMBA=MOTO.
7. MASHUKE= UDONGO.
8. MIZANI =UPEPO.
9. NGE=MOTO.
10. MSHALE=MOTO.
11. MBUZI =UDONGO.
12. SAMAKI = MAJI.
Kwa wale wasiojua tarehe zao za kuzaliwa namba zao za Bahati wanaweza kuzijua kwa herfi ya mwanzo ya jina lako maarufu au ulilopewa wakati unazaliwa kama ifuatavyo
A J S namba 1, B K T Namba 2, C L U Namba 3, D M V Namba 4, E N W Namba 5 F O X Namba 6, G P Y Namba 7, H Q Z Namba 8, na I R Namba 9
No comments:
Post a Comment