**
Unapofanya kitu unachokipenda siku zote utaishi maisha ya furaha.Lakini pia unapofanya kitu unachokipenda kwa muda mrefu kikashindwa kukuletea mrejesho mzuri hukuletea mfadhaiko na msongo mkubwa wa mawazo,hali hii ilimtokea "Vincent Van Gogh" msanii wa uchoraji kutoka nchini Uholanzi aliyewekeza nguvu na muda wake mwingi kwenye sanaa lakini ikashindwa kumnufaisha matokeo yake aliishi katika umaskini wa kupitiliza na mwishowe aliamua kujiua.Cha ajabu baada ya kujiua alipata umaarufu mkubwa sana michoro yake ilinunuliwa mamilioni ya fedha na kuwanufaisha watu wengine.Tuachane na "Van Gogh" tumtazame "Picasso,Pablo Picasso ni msanii aliyefanikiwa zaidi katika sanaa ya uchoraji na kumfanya aishi maisha ya kifahari kutokana na kipaji chake.Umahiri wake ulidhihirika pande zote za dunia hadi nguli wa muziki wa hip hop Shawn carter (Jay-Z) hakutaka kuficha hisia zake pale alipoamua kuingia studio kurekodi wimbo alioupa jina la "Picasso baby".Hii yote ni kuonyesha kuwa Pablo Picasso alijaaliwa kipaji maridhawa kilichomfanya sifa zake kuenea kila sehemu.Alizaliwa mwaka 1881 Malaga nchini Uhispania,alifundishwa kuchora na baba yake lakini katika umri mdogo baba yake alianza kuushangaa uwezo wa ajabu wa Picasso aligundua kuwa mwanae tayari amemshampita kiuwezo.Kwa nyakati tofauti aliwahi pia kuishi katika miji ya A Coruna,Barcelona na Madrid,katika harakati zake za kutafuta mafanikio kupitia sanaa muda wake mwingi akiwa mtu mzima aliishi Ufaransa.Kitu ambacho wengi hawakijui kuhusu Picasso ni kuwa aliwahi kufanya sanaa ya "katuni",mwaka 1901 Francisco de Asis Soler ambaye alikuwa rafiki wa Picasso alianzisha jarida lililoitwa "Arte Joven" katika jiji la Madrid.Picasso alichangia baadhi ya michoro katika jarida hilo kwa ushirikiano na wasanii wengine,aliifanya kazi hiyo kwa mafanikio ila aliendelea na kazi yake ya uchoraji wa picha za kawaida kwavile ndicho kitu alichokipenda zaidi.
No comments:
Post a Comment