** **
Walter Elias Disney,alizaliwa mwaka 1901 huko Chicago Illinois nchini Marekani,ni muasisi wa kampuni ya Walt Disney.Japo sanaa ya katuni ilishamiri zaidi karne ya 19 ila vyanzo mbalimbali vinaonyesha sanaa hiyo iligundulika tangu karne ya 16.Karne ya 19 ndiyo kipindi ambacho sanaa hiyo ya michoro ya kuchekesha ilianza kuchapishwa magazetini na kwenye majarida mbali mbali,pia wasanii kama "James Gillray" na wengineo walianza kujitokeza wazi wazi kipindi hicho.Katika masuala ya biashara "John Rockefeller" ndiye mfanyabiashara aliyefanikiwa zaidi katika historia,katika medani ya soka "Pele" ndiye mchezaji aliyefanikiwa zaidi na katika sanaa ya katuni ni Walt Disney.Anastahili kuiongoza kwa mafanikio tasnia ya sanaa ya katuni kulingana na changamoto nyingi alizozipitia katika maisha yake ya kisanaa.Pamoja na yote hakuruhusu changamoto yoyote ikatishe ndoto zake.Kitu kikubwa tunachoweza kujifunza kwake ni kuwa "kila changamoto inayokukabili ipo ndani ya uwezo wako".Mungu hajawahi kumpa mwanadamu changamoto iliyo nje ya uwezo wake hivyo ni vyema kujikita katika katafuta mbinu za kutatua changamoto zinazo tukabili.Mwaka 1940 Disney aliachia filamu zake mbili za katuni za Pinnocchio na Fantasia kipindi ambacho vita ya pili ya dunia ilikuwa tayari imeanza kupamba moto.Matokeo yake mapato yalishuka na alipata hasara katika filamu zake zote,aliingia katika madeni makubwa na benki ya Marekani.Alifanikiwa kujikwamua kutoka katika janga hilo na kufanikiwa zaidi.Hadi anafariki mwaka 1966 alikuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni $5, kwavile fedha ya zamani ilikuwa imara sana hicho ni kiasi kikubwa sana cha fedha ukilinganisha na thamani ya leo.
No comments:
Post a Comment