Mtambue Mnyama Asiyeshindwa "Nyegere"

Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe
Nyegere mojawapo ya chakula chao wanachopenda ni Asali. Anachofanya akiona Mzinga ana Ujambia na Nyuki hulewa kazi inayofuata ni kuanza kula asali. Ana ngozi ngumu sana hivyo kuchomwa na nyuki kwake ni kama anatekenywa.
Pia Nyegere anapenda Nyoka. Kwake nyoka hata awe anasumu yenye nguvu kiasi gani, Hapo anatafunwa kama kitumbua. Kwa nyoka wenye Sumu kali kama Koboko, baada ya kumla humlevya kwa dakika kadhaa ambapo atalala, kisha ataendelea na safari zake. Kutokana pia na ngozi yake si rahisi kudhurika lakini hata kama ataumwa bado sumu kwake si Chochote.

No comments:

Post a Comment

Active Visitors

Pages